#Local News

BUNGE LACHUNGUZA MALIPO YA SHILINGI BILIONI 6 KWA CHAMA CHA WAKUU WA SHULE

Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Umma inayoshughulikia elimu na utawala imeanza kuchunguza jinsi wakuu wa shule walivyolipa hadi shilingi bilioni sita kwa Chama cha Wakuu wa Shule za Sekondari nchini.

Wabunge wanahoji uhalali wa malipo hayo kwa chama hicho, huku wakuu wa shule za kundi la kwanza, zilizokuwa zikijulikana kama shule za kitaifa, wakikabiliwa na maswali kuhusu matumizi ya fedha na utunzaji wa hesabu.

Ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali imeonyesha udhaifu katika mifumo ya ndani ya udhibiti wa fedha katika baadhi ya taasisi hizo, huku kamati ya Bunge ikiendelea kuchunguza matumizi na usimamizi wa fedha hizo.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

BUNGE LACHUNGUZA MALIPO YA SHILINGI BILIONI 6 KWA CHAMA CHA WAKUU WA SHULE

TANKI LA MAFUTA LALIPUKA ELDORET

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *