#Local News

TANKI LA MAFUTA LALIPUKA ELDORET

Watu kadhaa wanahofiwa kufariki baada ya tanki la mafuta kulipuka katika barabara ya Eldoret-Turbo karibu na Shule ya Sekondari ya Paul Boit, katika tukio lililotokea Alhamisi usiku.

Shirika la Msalaba Mwekundu limesema watu kumi waliojeruhiwa wamepelekwa katika hospitali mbalimbali.

Hali hiyo ilidhibitiwa baada ya operesheni ya pamoja iliyohusisha wazima moto, huduma za ambulensi za kaunti, polisi, Msalaba Mwekundu pamoja na wananchi.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *