NDINDI NYORO AMTAKA RUTO KUACHA KUMSHAMBULIA UHURU
Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro amemjibu Rais William Ruto kuhusu kauli zake za mara kwa mara dhidi ya Rais mstaafu Uhuru Kenyatta, akimtaka rais kuangazia changamoto zinazowakabili Wakenya badala ya kuendelea kurejea masuala ya zamani.
Nyoro amesema Ruto hashindani na Uhuru bali anakabiliana na hali ya kiuchumi inayowakabili Wakenya, akidai ugumu wa maisha umeongezeka chini ya utawala wa sasa..
Nyoro pia amesema iwapo Ruto anatarajia kuheshimiwa atakapoondoka madarakani, anapaswa kwanza kumheshimu Uhuru akiwa bado rais, huku akimtaka kuangazia masuala yanayowahusu wananchi.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































