WADAU WA MAFUNZO YA UFUNDI WA KENYA NA ETHIOPIA WAMEKUTANA LEO JIJINI NAIROBI
Wadau wa elimu na mafunzo ya ufundi kutoka Kenya na Ethiopia wamekutana jijini Nairobi kujadili namna ujuzi wa kijani unavyoweza kusaidia vijana kupata ajira na kupunguza uchafuzi wa mazingira.
Mkutano huo uliandaliwa na Edukans Kenya kupitia mpango wa Wear the Green Future, kwa lengo la kutathmini mafanikio na changamoto za mradi huo unaolenga kuimarisha ujuzi wa vijana katika uhifadhi wa mazingira.
Mpango huo unashirikiana na vyuo vya ufundi na vituo vya mafunzo ya ufundi kuwafundisha vijana kutumia taka kama plastiki na nguo zilizotupwa kutengeneza bidhaa zinazoweza kutumika tena au kuuzwa, huku ukikuza ujasiriamali na fursa za ajira.
Imetayarishwa na Jesca Angeyo
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































