BABU OWINO, WEZAKE 6 WAONDOLEWA MASHTAKA
Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino na washtakiwa wenza 6 ambao ni Calvina Okoth maarufu kama Gaucho, Tom Ong’udi, Michael Omondi, Pascal Ouma, Kevin Wambo na Willys Baraka, wamepata afueni baada ya mahakama jijini Nairobi kukubali ombi la mkuu wa mashtaka ya umma kuwaondolea kesi ya uhalifu
Kwenye uamuzi huo, hakimu mkuu wa mahakama ya Milimani Lucas Onyina, amekiri kupitia ombi hilo kabla ya kukubali kuondoa kesi hiyo
Babu na wenzake walishtakiwa mwaka jana na mashtaka ya njama ya kutaka kuzua vurugu wakati wa maandamano yaliyoandaliwa na muungano wa Azimio.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































