#Local News

KIJANA AJINYONGA CHERANGANI, POLISI WAANZA UCHUNGUZI

Maafisa wa polisi wameanzish uchunguzi kuhusiana na kisa cha Kijana mmoja mwenye umri wa miaka 28 ambaye amejitoa uhai kwa kujinyonga katika eneo la Chepsiro Cherangani kaunti ya Transnzoia kufuatia kile kinakisiwa kuwa msongo wa mawazo usiku wa kuamkia leo.

Kulingana na chifu wa eneo hilo Gilbert Chepsiror mwendazake Aliakima Kipruto alikuwa mraibu wa pombe na kwamba alinusuriwa jana akitaka kujitumbukiza katika mojawapo ya mabwawa eneo hilo
Chepsiror aidha ametoa wito kwa vijana kutafuta ushauri nasaha wanapokumbwa na mafathaiko badala ya kujitoa uhai.

Imetayarishwa na Janice Marete

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *