VIJANA WACHUKUA MWELEKEO MPYA WA UCHAGUZI
Vijana nchini wameonyesha ari ya kuhakikisha sauti zao zinasikika kwenye uchaguzi mkuu ujao, kutokana na idadi yao kubwa ambayo sasa imeanza kujitokeza kusajiliwa kama wapiga kura, wakiapa kuwachagua viongozi walio tayari kuwajibika.
Katika siku za hivi karibuni, maelfu ya vijana wamejitokeza kusajiliwa na kusababisha changamoto kwa upande wa IEBC kushughulikia idadi ya juu, vijana hao wakijitokeza chini ya kauli mbiu: Tuko Kadi.
Vijana kote nchini wametakiwa kujitokeza katika vituo vya kusajiliwa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 
















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































