ATWOLI ATAKA UDHIBITI MKALI WA WAGENI NA MIPAKA YA NCHI
Katibu Mkuu wa COTU Francis Atwoli amesema kila nchi inapaswa kuwa na kumbukumbu za raia wa kigeni na kuhakikisha wana hati halali za kusafiria kama sehemu ya juhudi za kudhibiti uhalifu.
Atwoli amesema udhibiti wa mipaka ni muhimu ili serikali iweze kufahamu watu wanaoingia na kukaa nchini, huku akisisitiza umuhimu wa kuimarisha idara ya uhamiaji.
Amesema mataifa yanapaswa kulinda mipaka yao na kuweka mifumo madhubuti ya kufuatilia wageni, akitaja pia hitaji la kuhakikisha wageni wanaendelea kutambuliwa kwa mujibu wa sheria za uhamiaji.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































