#Local News

SERIKALI YA MAKUENI YAAHIDI KUSIMAMIA GHARAMA ZOTE ZA FAMILIA YA WATU7 WALIOKUFA KWA AJALI

Serikali ya Kaunti ya Makueni imesema itagharamia matibabu ya watu waliojeruhiwa katika ajali ya barabarani iliyotokea eneo la Kalembwani na kusababisha vifo vya watu saba papo hapo.

Zaidi ya watu 40 walijeruhiwa katika ajali hiyo na kupelekwa katika vituo mbalimbali vya afya kwa matibabu, huku serikali ya kaunti ikiahidi kugharamia matibabu yao.

Ajali hiyo imeibua tena wasiwasi kuhusu usalama wa barabarani, huku mamlaka husika zikitarajiwa kuchunguza chanzo cha ajali hiyo na kuchukua hatua za kuzuia matukio kama hayo kutokea tena.

Imetayarishwa na Hilda Ajema

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *