#Local News

OMOLLO: RASILIMALI ZA UMMA ZIFIKIE WAKENYA BILA UBAGUZI

Katibu Mkuu katika Wizara ya Usalama wa Ndani Raymond Omollo ametetea mkakati wa serikali wa maendeleo akisema rasilimali na huduma za umma zinapaswa kuwafikia Wakenya wote bila kuzingatia eneo, jamii au msimamo wa kisiasa.

Omollo amesema Rais William Ruto ameweka mkazo mpya wa uongozi unaolenga kuhakikisha jamii zote nchini zinanufaika na miradi na huduma za serikali bila ubaguzi.

Omollo pia amewakosoa wanaomkosoa Ruto na kuwataka Wakenya kuangalia miradi na maendeleo yanayotekelezwa huku wanaotafuta kura wakihitajika kutoa ahadi na mipango iliyo wazi kwa wananchi.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *