#Local News

WANDAYI ATETEA MPANGO WA G-TO-G KATIKA UAGIZAJI MAFUTA

Serikali imetetea mpango wa uagizaji mafuta wa serikali kwa serikali, ikisema mfumo huo una gharama nafuu, una hatari ndogo na ni rahisi katika uendeshaji.

Waziri wa Nishati Opiyo Wandayi amekanusha madai ya kuwepo kwa udanganyifu katika mpango huo, akitaja kampuni sita za ndani za uuzaji mafuta pamoja na benki saba zinazohusika.

Wandayi amesema kampuni hizo za ndani ziliteuliwa na mashirika ya kimataifa ya mafuta kushughulikia usafirishaji na shughuli nyingine za ndani, akisema serikali haingeweza kubadilisha uteuzi huo.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *