NG’ETICH AWEKA REKODI YA DUNIA KATIKA NUSU MARATHON COPENHAGEN
Mwanariadha wa Kenya Agnes Ng’etich ameandika historia katika Mashindano ya Dunia ya Mbio za Barabarani mjini Copenhagen Denmark baada ya kushinda mbio za nusu marathon kwa rekodi mpya ya dunia ya wanawake pekee ya saa 1 dakika 5 na sekunde 15.
Ng’etich amevunja kwa dakika moja na sekunde moja rekodi ya awali ya 1:06:16 iliyowekwa na Mkenya mwenzake Peres Jepchirchir mwaka 2020, huku Veronica Loleo akimaliza wa pili kwa muda wa 1:06:05 na kuipa Kenya nafasi mbili za kwanza.
Mwanariadha wa Rwanda Florence Niyonkuru alimaliza wa tatu kwa 1:06:08 huku Mkenya Daisilah Jerono akiwa wa nne kwa 1:06:13, huku ushindi huo ukimpa Ng’etich taji lake la pili la kimataifa msimu huu.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 




















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































