#Football #Sports

CUNHA AOKOA UNITED KATIKA SARE YA 1-1 DHIDI YA FULHAM

Manchester United ililazimisha sare ya 1-1 dhidi ya Fulham baada ya Matheus Cunha kufunga bao la kusawazisha dakika za mwisho, lakini matokeo hayo yameongeza presha kwa kocha Michael Carrick.

United ilihitaji ushindi katika uwanja wa Craven Cottage lakini ilijikuta nyuma katika kipindi cha pili baada ya Lisandro Martinez kujifunga wakati akijaribu kuzuia mpira kufuatia kipa Senne Lammens kuokoa shuti la Calvin Bassey.

Bao la Cunha limeizuia United kupata kichapo cha tatu mfululizo, lakini timu hiyo imeshinda mchezo mmoja pekee katika mechi tano za Ligi Kuu na sasa iko nyuma ya vinara Manchester City kwa pointi 10.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

CUNHA AOKOA UNITED KATIKA SARE YA 1-1 DHIDI YA FULHAM

CUNHA AOKOA UNITED KATIKA SARE YA 1-1

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *