#Local News

KINDIKI AMEWAJIBU WANAOMPINGA KUWA KIONGOZI MKUU WA JAMII YA AGIKUYU

Naibu Rais Profesa Kithure Kindiki amewajibu viongozi wa kisiasa wanaopinga kuidhinishwa kwake na wazee wa jamii za Agikuyu, Embu na Meru kuwa kiongozi mkuu wa kisiasa wa eneo la Mlima Kenya.

Kindiki aliidhinishwa Jumamosi na wazee hao kuongoza juhudi za kuleta umoja, maridhiano na maendeleo katika eneo hilo.

Akizungumza katika soko la Gaciongo, kaunti ya Tharaka Nithi, Kindiki amesema wazee hao wana mamlaka ya kitamaduni katika jamii hizo na viongozi wa kisiasa hawapaswi kupinga uamuzi wao wa kitamaduni.

Imetayarishwa na Jesca Angeyo

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *