POLISI WANACHUNGUZA KIFO CHA MWANAUME ANAYEDAIWA KUSHAMBULIWA KWENYE MGODI HUKO SIAYA
Maafisa wa polisi wanachunguza kifo cha mwanamume mwenye umri wa miaka 35 ambaye amefariki baada ya kudaiwa kushambuliwa kufuatia mzozo katika mgodi wa dhahabu wa Domba Agenda, eneo la Uyawi, Bondo, kaunti ya Siaya.
Marehemu anayetambuliwa kama Zachary Okeyo Odhiambo, anadaiwa kushambuliwa Jumamosi, Septemba 19, 2026 alipokuwa akifanya kazi katika mgodi huo.
Polisi wanasema uchunguzi unaendelea kubaini chanzo cha mzozo huo na waliohusika katika tukio hilo.
Imetayarishwa na Jesca Angeyo
English 






















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































