KARUA AWATAKA WAKENYA KUTETEA HAKI ZAO
Kiongozi wa chama cha PLP, Martha Karua, ametoa wito kwa wakenya kutetea haki zao kikamilifu huku chama cha wanasheria nchini LSK kikizindua wiki ya uhamasishaji wa kisheria 2025.
Hafla hiyo ambayo imeanza hii leo na inatarajiwa kuamilika tarehe 31, 2025, ambapo zaidi ya mawakili 18,000 wa Kenya wakitoa mashauriano ya kisheria bila malipo nchini kote.
Karua ameangazia vikwazo vya kimfumo kwa haki, akibainisha,dhuluma nyingi sana zinaendelea si kwa kukosa sheria, lakini zaidi kwa ukosefu wa ufahamu, uwakilishi, na wakati mwingine, ujasiri wa kuzingatia sheria kama ilivyo.
Imetayarishwa na Jones Koikai
English 






















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































