CHELSEA WAJIWEKA VYEMA UCL
Klabu ya Chelsea imejiweka kwenye nafasi nzuri katika michuano ya klabu bingwa barani Ulaya baada ya kuwashinda Pafos bao 1- 0 katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa Stamford Bridge. Bao la dakika ya 78 la Moises Caicedo liliwaweka Chelsea katika nafasi ya nane na hivyo kuwatia katika nafasi nzuri ya kufuzu moja kwa moja katika hatua ya pili. Matokeo Mengine yaliwaona Liverpool wakishinda Marseille ya Ufaransa Mabao 3-0, Newcastle wakawapiku Psv 3-0, Barcelona wakashinda 4-2 dhidi ya Slavia Praha wakati Juventus Wakiwapiga Benfica Mabao 2-0.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 






















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































