#Business

MGOMO WA WAFANYIKAZI WA SUKARI WASITISHWA

Mgomo wa nchi nzima wa wafanyikazi wa viwanda vya sukari umesitishwa kufuatia mazungumzo kati ya Serikali na Muungano wa Vyama vya Kupanda Sukari na Wafanyakazi Washirika nchini (KUSPAW).

Ukiongozwa na waziri wa Kilimo Mutahi Kagwe, mkutano uliofanyika katika jumba la Kilimo umeidhinisha kutolewa kwa shilingi bilioni 1 katika muda wa wiki mbili zijazo ili kupunguza matatizo ya mara moja kwa wafanyakazi.

Wafanyikazi walianza mgomo wao mwishoni mwa mwezi Januari mwaka huu wakitaka walipwe mishahara iliyosubiriwa na marupurupu ya jumla ya Ksh.10.8 bilioni. Kikao hicho kimeshughulikia kero hizo, kwani viongozi hao wamekubaliana kuwa malimbikizo yaliyobaki yatamalizwa kupitia Bajeti ya Nyongeza na Bajeti zinazofuata, zikisubiri kuidhinishwa rasmi na Bunge.

Imetayarishwa na Maurine Amwayi

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *