RUTO AAHIDI UCHAGUZI WA AMANI MWAKA 2027
Rais William Ruto amewahakikishia Wakenya kuwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2027 utakuwa wa amani, akiahidi serikali yake itachukua hatua kuhakikisha usalama unadumishwa kipindi chote cha uchaguzi.
Rais amesema serikali haitaruhusu makundi ya wahalifu kuingilia shughuli za kisiasa, akionya kuwa wote watakaohusika na vurugu, vifo au uharibifu wa mali watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Aidha, Ruto amesisitiza kuwa Kenya itaendelea kuwa taifa lenye amani, utulivu na umoja kabla, wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 






















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































