#Local News

MGOMO WA WAUGUZI WAZIDI KUVURUGA HUDUMA ZA AFYA

Tumaini la maelfu ya wagonjwa kupata matibabu katika hospitali za umma linaendelea kufifia, huku mgomo wa wauguzi na wakunga ukizidi kuathiri utoaji wa huduma za afya katika kaunti mbalimbali.

Wauguzi na wakunga wanaendelea na mgomo ulioingia siku ya pili, hali iliyosababisha huduma za afya kusimama katika hospitali nyingi za umma nchini.

Wagonjwa walikosa matibabu katika kaunti za Kericho, Kisumu, Machakos, Embu, Tharaka Nithi na maeneo mengine baada ya hospitali nyingi kushindwa kutoa huduma kutokana na mgomo huo.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *