SERIKALI YATETEA MSWADA MPYA WA UFADHILI WA ELIMU YA JUU
Serikali imetetea mapendekezo ya mabadiliko katika ufadhili wa elimu ya juu, ikisema yanalenga kuongeza idadi ya wanafunzi wanaojiunga na vyuo vikuu na taasisi nyingine za elimu ya juu.
Wizara ya Elimu imeambia Kamati ya Elimu ya Bunge la Kitaifa kuwa Mswada wa Uteuzi na Ufadhili wa Elimu ya Juu utasaidia kufanikisha lengo la serikali la kuhakikisha wanafunzi wote wanaohitimu wanapata nafasi ya kuendelea na masomo.
Maafisa wakuu wa wizara wamesema mfuko huo utagharamiwa kupitia ruzuku ya serikali, mikopo ya masoko ya mitaji, akiba ya wazazi, marejesho ya mikopo ya wanafunzi na mikopo nafuu, huku mahitaji ya ufadhili yakitarajiwa kufikia shilingi bilioni 230 kwa mwaka ifikapo 2030.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 






















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































