MGOMO WA WAFANYIKAZI WAKWAMISHA SAFARI ZA NDEGE NCHINI
Mamia ya wasafiri wamekwama katika viwanja mbalimbali vya ndege nchini baada rubani na wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege kuanza mgomo wakishinikiza kuboreshwa kwa maslahi na mazingira ya kazi
Wafanyakazi hao pia wanataka serikali kutekeleza makubaliano ya awali kuhusu marupurupu na mafao yao ya kikazi, wakisema masuala hayo hayajashughulikiwa licha ya makubaliano yaliyofikiwa
Mgomo huo umevuruga shughuli za usafiri wa anga, huku mashirika kadhaa ya ndege yakilazimika kuchelewesha au kubadilisha ratiba za safari, hali inayowaacha abiria wakisubiri suluhu.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 






















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































