#Local News

RUTO NA RUBIO WAKUBALI KUIMARISHA USHIRIKIANO WA KENYA NA MAREKANI

Rais William Ruto amekutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio mjini New York, ambapo wamejadili namna ya kuimarisha ushirikiano wa Kenya na Marekani katika biashara, teknolojia, madini muhimu, nishati na usalama wa kikanda.

Mkutano huo ulifanyika pembeni mwa Mkutano wa 81 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, huku Kenya ikilenga kuimarisha zaidi uhusiano wake wa kiuchumi na kimkakati na Marekani.

Ruto amesema uhusiano kati ya Kenya na Marekani umejengwa katika misingi ya biashara, usalama, teknolojia na maendeleo, akisisitiza umuhimu wa kuendeleza ushirikiano huo.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *