#Local News

NDINDI NYORO AJIUNGA NA UPINZANI

Huku joto la kisiasa likizidi kupanda nchini kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027, Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro ametangaza kujiondoa upande wa serikali na kujiunga rasmi na upinzani akilalamikia ukosefu wa uwajibikaji katika utawala wa sasa

Nyoro amesema yeye pamoja na wafuasi wake wamejiunga na chama cha People’s Party of Kenya, akitangaza kuwa chama hicho sasa kitashirikiana rasmi na kambi ya upinzani.

Hatua hii inajiri baada ya kuzuka kwa maswali kuhusiana na msimamo kamili wa Nyoro kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *