#Local News

KINDIKI AWATAKA VIONGOZI WA MOUNT KENYA KUHESHIMU WAZEE NA WITO WA UMOJA

Naibu Rais Kithure Kindiki amewataka viongozi wa eneo la Mlima Kenya kuwaheshimu wazee na kuzingatia wito wao wa kuunganisha jamii, akisema tofauti za kisiasa hazifai kugawanya watu wenye historia na maslahi ya pamoja.

Akizungumza Tharaka, Kindiki amesema wazee wana nafasi ya kipekee katika kulinda umoja wa jamii kwa kuwa hawashindanii nyadhifa za kisiasa wala ushawishi wa kisiasa, hivyo maamuzi na ushauri wao unapaswa kuheshimiwa.

Kindiki pia amepuuzilia mbali madai ya wapinzani wake kwamba hafai kuwa msemaji wa jamii hiyo kufuatia kutawazwa kwake na wazee wa eneo la Mlima Kenya.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *