#Football #Sports

HUSSEIN MOHAMMED ATOA WITO WA SULUHISHO KATIKA MGOGORO WA LIGI

Rais wa Shirikisho la Soka nchini  Hussein Mohammed ametoa wito wa kupatikana kwa suluhisho la kisiasa katika changamoto za kisheria zinazochelewesha kuanza kwa Ligi Kuu ya Kenya msimu wa 2026/27.

Hussein amesema mchakato wa kisheria unaweza kuchelewesha zaidi ligi, huku Kariobangi Sharks na Mombasa United zote zikidai nafasi katika msimu huo, baada ya mahakama mbili kutoa maagizo yanayokinzana kuhusu namna ligi inavyopaswa kuendeshwa.

Mombasa United ilimaliza nafasi ya tatu katika Ligi ya Taifa ya Daraja la Kwanza, huku kanuni za Shirikisho za mwaka 2019 zikielekeza ikabiliane na Kariobangi Sharks iliyomaliza nafasi ya tatu kutoka mwisho katika Ligi Kuu, kwa nafasi ya kucheza msimu wa 2026/27.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *