MOHAMED SALAH AREJEA LIVERPOOL
Mohamed Salah alirejea kwenye kikosi cha Liverpool, kufuatia kuwakilisha Misri kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika, huku klabu ikiendeleana maandalizi ya mchezo wa Champions League dhidi ya Marseille.
Salah, akiwa na tabasamu, alifanyiwa mazoezi katika kituo cha mafunzo cha klabu pamoja na wachezaji wengine wote wa Arne Slot kabla ya mchezo wa leo nchini Ufaransa.
Kurudi kwa mshambuliaji huyo wa Misri kumeibua mjadala mkubwa, hasa baada ya mahojiano yenye hasira aliyoyatoa mwanzoni mwa mwezi uliopita akieleza malalamiko yake dhidi ya Liverpool.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 

































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































