#Football #Sports

MKUFUNZI WA TUSKER FC AAHIDI MWAMKO MPYA KLABUNI

Kocha mkuu mpya wa klabu ya Tusker FC, Mfaransa Julien Mette, amesema kuwa klabu hiyo haitazuilika tena punde baada ya wachezaji wake kujifahamisha na mtindo na falsafa yake ya mchezo.

Mette ameonyesha kuridhishwa na jinsi wachezaji wake wanavyokumbatia mtindo na mbinu zake, anapojiandaa kwa mechi yake ya pili hii leo dhidi ya Murang’a Seal katika uwanja wa Wang’oru saa nane mchana.

Kocha huyo alionjeshwa kichapo kwenye mechi yake ya kwanza Jumamosi, vijana wake walipochabangwa bao 1-0 na Shabana FC.

Mfaransa huyo atalenga kuiongoza timu hiyo kuandikisha ushindi muhimu leo, hasa baada ya kuandikisha ushindi mmoja pekee katika mechi 5 za zilizopita za ligi.

Kwa sasa wanashikilia nafasi ya 10 kwa pointi 28 baada ya mechi 21, pointi 18 nyuma ya viongozi Gor Mahia.

Mechi nyingine itakayosakatwa hii leo ni kati ya Nairobi United na Bandari FC, na Shabana FC dhidi ya Mathare United.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

MKUFUNZI WA TUSKER FC AAHIDI MWAMKO MPYA KLABUNI

KESI YA MAUAJI DHIDI YA AFISA WA

MKUFUNZI WA TUSKER FC AAHIDI MWAMKO MPYA KLABUNI

KVF: KCB UGANI DHIDI YA SPIKERS

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *