#Local News

UTABIRI: MVUA KUONGEZEKA IJUMAA

Mvua inayoendelea kwa sasa katika maeneo mbali mbali ya nchi inatarajiwa kuongezeka na kufikia mililita 20 kati ya leo na Jumanne wiki ijayo, wananchi wakionywa kuhusu uwezekano wa mafuriko ya ghafla.

Katika utabiri wake, idara ya utabiri wa hali ya anga imesema maeneo yatakayoathirika ni pamoja na kaunti za Turkana, West Pokot, Samburu, Migori, Bungoma, Nyamira, Busia, Vihiga, Trans Nzoia, Kakamega, Nandi, ukanda wa pwani, Ukambani na Kaskazini Mashariki.

Aidha, imesema mvua hiyo itafikia kilele kati ya kesho na Jumatatu kabla ya kupungua na kuendelea taratibu.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *