GACHAGUA: DCI HAIWEZI KUJICHUNGUZA
Idara ya upelelezi wa jinai DCI imetakiwa kujiondoa kwenye uchunguzi unaoendelea katika Sakata ya mafuta iliyosababisha kupotea kwa shilingi bilioni 2.9, kwa misingi kwamba ilihusika katika uagizaji wa mafuta hayo.
Kiongozi wa chama cha DCP Rigathi Gachagua, amesisitiza kwamba idara hiyo ni mwanachama wa kamati ya kitaifa ya usalama, NSAC, na hivyo itavuruga uchunguzi huo ikizingatiwa kuwa washukiwa wakuu wametaja kuhusika kwa kamati hiyo katika Sakata hiyo.
Gachagua ametaka uchunguzi huru kufanywa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 


































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































