SIFUNA AONDOLEWA NAFASI YA NAIBU MJELEDI WA WACHACHE SENETI
Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna ameondolewa katika wadhifa wa Naibu Kiranja wa Wachache katika seneti Seneti kufuatia hatua mpya ya chama cha ODM dhidi yake.
Katika taarifa iliyowasilishwa bungeni na Spika wa Seneti Amason Kingi, Seneta wa Migori Eddy Oketch alitangazwa mara moja kuchukua nafasi hiyo.
Mabadiliko hayo yamekuja baada ya mkutano wa maseneta ulioripotiwa kufanyika katika ofisi ya Kiranja wa Wachache Ledama Ole Kina, huku uamuzi huo ukiendelea kupingwa na kiongozi wa Azimio Kalonzo Musyoka.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 





























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































