BASKETBALL: KPA YALENGA KUIMARISHA SAFU YA ULINZI LICHA YA MATOKEO MAZURI
Kocha wa Kenya Ports Authority (KPA), Robert Mugabe, amesema timu yake itaendelea kuboresha safu ya ulinzi licha ya kupata ushindi mara mbili mfululizo katika Ligi Kuu ya Mpira wa Kikapu kwa Wanaume.
KPA iliichapa Moischers kwa alama 88-57 kabla ya kuifunga ANU Wolfpacks kwa 89-70, katika mechi zilizochezwa mwishoni mwa wiki katika viwanja vya USIU.
Mugabe amesema safu ya ushambuliaji inaonyesha maendeleo mazuri kwa kutengeneza nafasi nyingi za kufunga, lakini amesisitiza kuwa kipaumbele sasa ni kuimarisha ulinzi kuelekea mechi zijazo.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 

































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































