JUNET ADAI WABUNGE WALIHONGWA KUMNG’OA GACHAGUA
Mbunge wa Suna Mashariki, Junet Mohammed, amedai kuwa wabunge walipokea pesa kabla ya kupiga kura ya kumng’oa aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua madarakani mwezi Oktoba 2024.
Akizungumza katika mkutano wa pamoja wa vyama vya UDA na ODM uliofanyika Kakamega, Junet alidai kuwa fedha zilitolewa kwa baadhi ya wabunge wa Bunge la Kitaifa na Seneti kabla ya kupitishwa kwa hoja ya kumwondoa Gachagua.
Aidha, Junet alidai kuwa baadhi ya wabunge hawakutumia pesa hizo ipasavyo, akiwashauri kujenga nyumba bora badala ya kuzitumia kwa mambo mengine.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































