SERIKALI YAJIPANGA KUKABILIANA NA EL NIÑO
Wakati utabiri wa hali ya Hewa ukionyesha dalili za mvua kubwa ya El Nino, Waziri wa Utumishi wa Umma Geoffrey Ruku, amesema kuna uwezekano wa asilimia 80 wa nchi kushuhudia mvua za El Niño kati ya mwezi Oktoba na Desemba mwaka huu.
Ruku amesema serikali imeunda kamati maalumu inayoongozwa na Naibu Rais Kithure Kindiki ili kuratibu maandalizi ya kitaifa kabla ya kuanza kwa mvua hizo.
Aidha, amesema maandalizi hayo yanalenga kupunguza athari zinazoweza kusababishwa na El Niño na kuhakikisha nchi iko tayari kukabiliana na hali hiyo.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 






















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































