#Football #Sports

GOR MAHIA WAJIPANGA KWA NUSU FAINALI YA KAGAME CUP DHIDI YA AL HILAL

Gor Mahia  wameendelea kuimarisha maandalizi yao kuelekea nusu fainali ya mashindano ya CECAFA Kagame Cup watakayocheza dhidi ya Al Hilal Omdurman siku ya Jumanne.

Mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Kenya waliongoza Kundi A na kufanya mazoezi makali Jumapili chini ya kocha Charles Akonnor, wakilenga kujiandaa vyema kwa pambano hilo muhimu.

Al Hilal walifuzu kwa hatua ya nusu fainali licha ya kupoteza mchezo wao wa mwisho wa Kundi C dhidi ya Rayon Sports, jambo linalotarajiwa kufanya pambano hilo kuwa la ushindani mkubwa.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *