RUTO ATETEA UCHUMI WA NCHI
Rais William Ruto ameeleza hatua ambazo serikali imechukua katika kuimarisha uchumi, wakati wa kikao cha serikali jumuishi jijini Naivasha.
Ruto ametetea rekodi ya serikali katika uchumi, akisema mpango wa Nyumba za Bei Nafuu umesaidia kukabiliana na ukosefu wa ajira pamoja na uhaba wa makazi.
Rais Ruto amesema serikali imeendelea kuelekeza rasilimali katika sekta muhimu za uchumi, akisisitiza kuwa uwekezaji huo unalenga kuchochea ukuaji wa uchumi na kuboresha maisha ya wananchi.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 

































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































