#Local News

TANDAZA: RUWAZA 2060 ITATOKA KWA WAKENYA

Mbunge wa Matuga Kassim Tandaza ametetea Ruwaza 2060 akisema tofauti yake kuu na Ruwaza 2030 ni kuwa mpango huo mpya utaongozwa na wananchi kupitia ushirikishwaji mpana wa umma

Tandaza amesema mchakato huo utawapa Wakenya nafasi ya kutoa maoni na kuamua vipaumbele vya maendeleo ya muda mrefu wanavyotaka kuona nchini

Amesema Ruwaza 2060 inapaswa kuzingatia misingi ya Katiba ya mwaka 2010 hasa hitaji la wananchi kushirikishwa katika maamuzi yanayohusu mwelekeo wa taifa

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *