#Football #Sports

MAN CITY YAANZA ENZI MPYA KWA USHINDI WA KUSISIMUA

Manchester City imeanza maisha bila Pep Guardiola kwa ushindi wa dakika za mwisho, ikiilaza Bournemouth 2-1 katika mechi ya kwanza ya Ligi Kuu chini ya kocha mpya Enzo Maresca.

Bournemouth ilionekana kuelekea kuvuruga sherehe za City baada ya Marcus Tavernier kuifungia bao la kuongoza kipindi cha kwanza katika uwanja wa Etihad, lakini wenyeji wakaanza kurejea kwa nguvu dakika za mwisho.

Marc Guehi alisawazisha kwa kichwa zikiwa zimesalia dakika sita, kabla ya Josko Gvardiol kuifungia City bao la ushindi katika muda wa nyongeza na kuanzisha enzi mpya kwa kishindo.

Katika Matokeo Mengine Arsenal waliwalaza Coventry 3-0, Man United wakaduwazwa na Hull City 2-0,Tottenham Wakadhalilishwa 3-0 na Brentford wakati Liverpool wakitoka sare ya 2-2 na Newcastle United.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *