RAIS WILLIAM RUTO AKIRI KUWA WAKENYA WANA HAKI YA KUANDAMANA
Rais William Ruto amesema kuwa wakenya wana haki ya kuandamana na kutoa maoni yao kwa njia ya amani akisema maandamano ya upinzani ni nguzo muhimu za demokrasia.
Akizungumza katika kongamano la 16 la siku ya katiba lililoandaliwa katikaukumbi wa KICC jijini Nairobi Ruto ametafakari kuhusu maandamano yalioongozwa na vugu vugu la vijana wa Gen Z mwaka 2024 na maswala ya kikatiba yaliyoibuliwa na maandamano hayo.
Rais aidha amesema vijana na wakenya wengine walitumia haki zao za kikatiba kuzungumza, kukusanyika , kuandamana na kupiga kura ya maoni kwa kuwasilisha malalamishi yao kwa mamlaka za umma.
Imetayarishwa na Hilda Ajema
English 

































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































