#Local News

MWANAMKE AUWAWA KWA RISASI NA POLISI UASIN GISHU

Tukio la kushtua limetokea katika eneo la Naiberi, kaunti ya Uasin Gishu, baada ya mwanamke mwenye umri wa miaka 45, Doris Murei, kupigwa risasi na afisa wa polisi katika eneo la GSU Mess, kufuatia mabishano yaliyoibuka kati yao

Mashuhuda wamesema tukio hilo lilitokea Jumapili majira ya saa kumi na moja jioni, huku polisi wakieleza kuwa afisa huyo aliyekuwa na bunduki alidaiwa kumpiga risasi Murei wakati wa makabiliano, na kumuua papo hapo

Afisa huyo, anayesemekana kuwa miongoni mwa walinzi waliokuwa wameambatanishwa na gavana, alitoroka eneo la tukio baada ya ufyatuaji huo, huku polisi wakianzisha msako wa kumkamata na kubaini chanzo cha mabishano hayo.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *