WASHUKIWA WATATU ZAIDI WAKAMATWA KWA MAUAJI YA DKT MUTISO
Washukiwa wengine watatu, akiwemo afisa wa polisi, wamekamatwa kuhusiana na mauaji ya Dkt Victoria Mutiso, huku wawili wakikamatwa jijini Kampala nchini Uganda na mwingine akinaswa eneo la Lang’ata jijini Nairobi
Afisa huyo wa polisi anayehudumu katika Kituo cha Polisi cha Thogoto anadaiwa kuwa ndani ya moja ya magari yaliyotumiwa kuzuia teksi aliyokuwa akisafiria Dkt Mutiso kabla ya kuuawa, huku uchunguzi ukiendelea kubaini kila aliyehusika
Washukiwa waliokamatwa Uganda wanazuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Jinja Road jijini Kampala wakisubiri kurejeshwa nchini Kenya, huku polisi wakiendelea na uchunguzi wa tukio hilo.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 


































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































