#Local News

OLUGA: HAKUNA MAMA AU MTOTO ANAYEFAA KUFARIKI KWA SABABU ZINAZOZUILIKA

Katibu Mkuu katika wizara ya afya Ouma Oluga amesema hakuna mwanamke wala mtoto anayefaa kupoteza maisha kutokana na sababu zinazoweza kuzuilika, akisisitiza dhamira ya serikali kuboresha afya ya kina mama na watoto wachanga.

Oluga amesema serikali inaendelea kuweka mikakati ya kupunguza vifo vya kina mama na watoto wachanga kupitia mpango wa kuhakikisha kila mama na kila mtoto anapata huduma muhimu za afya.

Amesema hatua hiyo inalenga kuimarisha huduma za afya ya uzazi na kuhakikisha changamoto zinazoweza kuzuilika hazisababishi tena vifo vya kina mama na watoto wakati wa ujauzito, kujifungua na baada ya kujifungua.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *