#Local News

KRA IMEBAINI UDANGANYIFU WA FORODHA YA SIMU 55,000 KATIKA UWANJA WA NDEGE WA ELDORET

Mamlaka ya Mapato Kenya, KRA, imebaini udanganyifu mkubwa wa forodha katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Eldoret baada ya kugundua simu zaidi ya elfu 55,000 katika mzigo uliokuwa umetangazwa kuwa na simu elfu 3 pekee.

Uchunguzi wa KRA umebaini kuwa simu elfu 52,607 za kawaida hazikutangazwa, huku simu nyingine 309 za bei ya juu zikiwa hazikutangazwa kabisa kwa forodha.

KRA inakadiria kuwa serikali huenda ilipoteza mapato ya shilingi milioni 50 nukta 4 kutokana na kutotangazwa kwa simu hizo.

Imetayarishwa na Jesca Angeyo

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *