KENYA YAAHIDI KUWATUMA POLISI ZAIDI HAITI
Kenya imeahidi kuwatuma maafisa wengine 600 wa polisi katika taifa la Haiti wiki zijazo ili kushirikiana na wenzao waliotangulia katika kupambana na magenge ambayo yanadhibiti maeneo muhimu ya taifa hilo, likiwemo jiji kuu la Port-au-Prince.
Idadi hiyo itafikisha jumla ya polisi 1,000 walioahidiwa kuwasilishwa nchini humo kusaidia kurejesha utulivu, kwa ushirikiano na vikosi kutoka mataifa mengine ambayo yameahidi kuwatuma maafisa 1,900 wa polisi kwa pamoja.
Akizungumza baada ya kuwatembelea polisi wa Kenya nchini Haiti, Rais William Ruto amepongeza juhudi za polisi hao hadi sasa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 

































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































