#Local News

RUTO ATAKA MABADILIKO KATIKA MFUMO WA FEDHA DUNIAN

Rais William Ruto ametaka mabadiliko ya msingi katika mfumo wa fedha duniani na utawala wa kimataifa, akisema akiba za ndani za Afrika hazitumiki ipasavyo kuchochea maendeleo ya bara.

Akizungumza katika mkutano wa Kenya na Umoja wa Ulaya kuhusu ushirikiano wa pande nyingi mjini New York, Ruto amesema Afrika ina akiba ya kutosha ya ndani kuendeleza mipango yake ya maendeleo.

Hata hivyo, amesema rasilimali hizo za kifedha bado hazitumiki kikamilifu na kuitaka Afrika kubuni mifumo itakayowezesha mataifa yake kukusanya na kutumia rasilimali hizo kwa maendeleo.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *