ABUD OMAR AONYA KENYA KUBAKI NYUMA KISOKA KULIKO MAJIRANI
Nahodha wa Tusker Abud Omar amesema soka la Kenya linazidi kubaki nyuma ya nchi jirani, akitaja usimamizi duni, ukosefu wa miundombinu na kutokuwepo kwa weledi kama changamoto zinazoikumba ligi ya humu nchini.
Omar ametoa kauli hiyo baada ya kuahirishwa tena kwa Ligi kuu ya humu nchini, hali ambayo imeviacha vilabu na wachezaji bila uhakika kuhusu lini msimu wa 2026/2027 utaanza.
Msimu huo ulitarajiwa kuanza Septemba 19 lakini ukaahirishwa kutokana na hatua mpya za kisheria kuhusu muundo wa ligi pamoja na mfumo wa kupandisha na kushusha timu, huku Omar akisema soka la Kenya lilikuwa katika hali bora zaidi miaka kumi iliyopita.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 








































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































