#Football #Sports

MBAPPE AKOSA MAZOEZI KABLA YA MECHI YAKE YA KWANZA CHINI YA ZIDANE

Nahodha wa Ufaransa Kylian Mbappe amekosa mazoezi ya timu hiyo baada ya kuonyesha dalili za mafua, hali inayotia shaka ushiriki wake katika mechi zijazo za Ligi ya Mataifa.

Mshambuliaji huyo wa Real Madrid alibaki katika kambi ya timu huku wachezaji wengine wakifanya mazoezi chini ya kocha mpya Zinedine Zidane, anayejiandaa kwa mechi yake ya kwanza dhidi ya Uturuki Ijumaa.

Ufaransa pia inatarajiwa kucheza dhidi ya Ubelgiji nyumbani na ugenini pamoja na Italia katika kipindi hiki cha kimataifa, huku hali ya Mbappe ikiwa changamoto ya mapema kwa Zidane.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *