ANGUKA PEKEE YAKO, UDA KWA MALALA
Chama cha UDA kupitia kwa kaimu katibu mkuu Hassan Omar kimemuonya aliyekuwa kaimu katibu mkuu wa chama hicho Cleophas Malala kutohusisha masaibu yake na mwenyekiti wa UDA Cecil Mbarire na kiongozi wa walio wengi bungeni Kimani Ichung’wa.
Kupitia taarifa, Omar amepuzilia mbali madai ya Malala kwamba kulikuwa na njama ya kumbandua kutoka mamlakani naibu rais Rigathi Gachagua, akisema Mbarire hangehusika kwani yeye si mbunge.
Aidha, Omar ameshikilia kwamba Malala alitimuliwa kisheria, na uamuzi huo kuidhinishwa na msajili wa vyama vya kisiasa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 








































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































