#Local News

DKT PETER MBAE WA DCP AMESEMA UPINZANI HAUTAMTANGAZA MGOMBEA WAKE WA URAIS KABLA YA MWISHO WA MWAKA

Katibu wa Mipango na Masuala ya Kiuchumi wa Chama cha Democracy for Citizens Party (DCP), Dkt. Peter Mbae, amesema upinzani hautamtangaza mgombea wake wa pamoja wa urais kabla ya mwisho wa mwaka huu.

Dkt. Mbae amesema vyama vya upinzani bado vinaendelea na mashauriano kuhusu namna ya kuunganisha nguvu kuelekea uchaguzi mkuu ujao.

Amesema mchakato huo unahitaji muda ili vyama hivyo kufikia mwafaka kuhusu mgombea wa pamoja pamoja na masuala mengine ya ushirikiano.

Imetayarishwa na Jesca Angeyo

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *