AMBANI ALENGA KUSHINDA LIGI YA FKF NA AFC LEOPARDS
Kocha wa AFC Leopards, Fred Ambani, amesema wachezaji wapya waliosajiliwa wana uwezo wa kuirejesha timu hiyo kileleni na kumaliza ukame wa miaka 27 bila kutwaa taji la Ligi Kuu ya FKF.
Ambani amesema mshambuliaji mpya kutoka Gambia, Musa Ceesay, ataleta makali yaliyokosekana katika safu ya ushambuliaji msimu uliopita, huku akieleza kuwa mchango wake utakuwa muhimu katika harakati za timu.
Aidha, kocha huyo amesema ufadhili wa shilingi milioni 25 uliotolewa kwa klabu hiyo umeipa nafasi ya kuimarisha kikosi, akisisitiza kuwa lengo lao ni kurejesha hadhi ya AFC Leopards na kuiondoa Gor Mahia kileleni mwa soka la Kenya.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































